Natazama nyuma, mawazo yangu yanagota mwaka 2010, nikiwa mwanafunzi wa kidato cha pili.
Ni mchana baada ya chakula, hakuna mwalimu darasani, natoka naketi pembezoni mwa darasa na daftari langu la Kemia kujisomea.
Hatua kadhaa mbele yangu ni ukuta wa shule. #UZI
#DaktariMwandishi
Nje ya ukuta huo kuna mti wa mwembe unaochungulia ndani ya ukuta ma kamlima kidogo, ni barabara wanayopita wanafunzi wa shule za kata za jirani, Kwembe na Luguruni.
Nikiwa nimezama katika notes zangu, naisikia sauti ikiita, "Angel, Angel"
Nainua macho yangu kuona wanafunzi watatu
wa Kwembe wa kiume wamesimama kwenye kale kamlima.
"Mimi sio Angel, nikawaitie?", nawajibu.
"Ndio, katuitie Angel form 2", akajibu mmoja wao.
Nilijua wazi hatukuwa na mwanafunzi aitwaye "Angel", tulikuwa na Angela.
Nikainuka kwenda darasani, nikamchukua Melissa, nikampanga.
Akaja wakamfurahia, wakimuita Angel. Tukajua basi, ni waongo tu.
Siku ikakata. Tukasahau yaliyotokea.
Kesho yake nikiwa nimeketi pale pale, wakaja tena, wakimuulizia Angel. Nikawauliza tena, "nikawaitie?"
Wakakataa katakata wakisema mimi ndio Angel.
Nikakubali ili yaishe.
Na hapo
nikaianza safari iliyobadilisha maisha yangu.
Ikawa karibu kila siku nikiketi pale, walipita na kunisalimu.
Siku nyingine walikimbizwa na walinzi.
Tukajenga urafiki.
Majina yao, Chris, Frank na Nurdin.
Wakati huo tunakaribia mtihani wa taifa wa kidato cha pili, tumeshazoeana.
Walikuwa wanatungua maembe na kunirushia. Naosha nakula. Utoto bwana!
Siku moja, Nurdin akachukua chingwa bichi, akaandika namba zao za simu, akalirusha. Nikalitunza.
Na mimi nikawaandikia kwenye karatasi possible za essay na topics muhimu zinazoweza kutoka kwente NECTA,
nikawarushia.
Tukafanya NECTA, tukarudi nyumbani.
Tukaanza kuwasiliana. Tukawa marafiki wakubwa.
Miaka ikaenda. Wakawa wanakuja shuleni kunitembelea siku ya Visitation na Graduation, hakika unajua mavazi ya vijana enzi hizo supra zipo moto, mama hakufurahishwa kabisa.
Wakati wa likizo, tulikwenda wote tuition Mapambano, wao bata nyingi walikuwa wanadoji, mimi nakomaa.
Siku zisizo za tuition walikuwa wakija nyumbani, tunakaa dinning tunadiscuss na kusolve maswali, mama anatusimamia.
Anahakikisha kila mmoja anachangia.
Hakika tulikuwa tunatoka
katika shule tofauti sana lakini urafiki tulioujenga ulinawiri siku hadi siku.
Kadri siku zilivyokwenda, jina Angel likawa si geni kwenye midomo ya wanafunzi wengi wa Kwembe na Luguruni.
Hata siku ya Graduation yangu, walikuja kama 10 hivi, wakanipa na zawadi.
Tukamaliza form 4.
Ni mwaka 2012, hakika hakuna atakayesahau matokeo haya. Yalitisha. Yalisikitisha.
Bahati mbaya, wenzangu wote hawakufaulu. Mimi nilifanikiwa kufaulu.
Nafahamu mengi yalichangia hilo kutokea.
Tukaanza kupotezana kidogo kidogo, lakini mmoja, Frank, tukaendelea kuwasiliana kwa
ukaribu. Nikamshauri Frank, a-reseat mtihani wa form 4, asiiache elimu. Akakubali.
Nikajitahidi kumpa kila notes na maswali aliyohitaji na kumtia moyo asichoke.
Mara ya kwanza, akafeli tena.
Ya pili, akafeli.
Ya tatu, akafaulu.
Akapata cheti cha form 4.
Nikafurahi sana.
Akaianza
safari mpya ya maisha yake.
Tukaendelea kuwasiliana, na nikiwa mwaka wa kwanza chuo, siku ya Birthday yangu, nikapokea simu yake, "Best, jiandae tukale nyama"
Sikuwa mtu wa kutoka, hivyo nikasema, sawa.
Akaja na gari, akanichukua tukaenda, nikakuta surprise ya keki na champagne.
Tukasherehekea, na hii ndio Birthday ya pekee niliyosherehekea nikiwa chuo.
Akaniambia wakati huo, anafanya kazi shirika la Ndege.
Alijiendeleza kozi mbalimbali zinazohusiana na masuala ya Anga na Cargo, na sasa ameajiriwa.
Amefanikiwa kumsomesha mdogo wake na kuwasaidia watoto
wengine wawili wasiojiweza.
Sikuamini. Alipendeza. Alivaa kiutanashati. Hakuwa Frank yule wa enzi za Kwembe.
Nilimtazama, nikakumbuka siku ile ya graduation yangu walipowasili tukiwa katikati ya sherehe, wakiwa wanashuka ngazi, wenzangu wakaanza kushangilia, Kwembe boys wamefika.
Walikuwa wamevaa miwani, na suti za rangi za kung'aa, yani popote pale ni rahisi kuwaona.
Nilibatizwa jina la "Queen of Kwembe"
Nikikumbuka nacheka sana.
Baada ya mazungumzo na kufurahia keki na champagne, akanifahamisha kuwa alikuwa anafuatilia kwenda kujiendeleza kimasomo zaidi
Nilikuwa proud sana. Hakika Frank alikuwa amekua, amebadilika na anaifuatilia future yake.
Tukapiga stori, huku akiiga sauti yangu nilivyokuwa nawalalamikia enzi hizo, "twendeni tuition, twendeni tukasome"
Tukacheka sana.
Maneno yake yakanigusa kwa namna yake, akasema
"Unajua best, sijui uliona nini ndani yetu. Lakini ulichokiona, kimenipa ujasiri wa kufika hapa leo."
Kiukweli, hata mimi mwenyewe sijui. Kwangu, niliamini kila mtu ana nafasi ya kujenga future yake bila kujali alipotoka au shule aliyosoma.
Ndio maana nilijitahidi kuwatia moyo.
Leo hii, Frank anaendelea na masomo yake Afrika Kusini, amekuwa mfanyakazi mzuri na amepata mafanikio sana.
Namtazama, nafurahi sana kwasababu nimemfahamu tangu enzi hizo ananitungulia maembe na kukimbizwa na walinzi kwa kuongea na mimi.
Isingekuwa COVID19, angekuwa anakaribia
kumaliza kabisa.
Insha'Allah, namuombea amalize na azidi kufanikiwa.
Maisha ya Frank, yamenifundisha kitu kikubwa sana.
Tofauti na baadhi yetu tuliozaliwa na kijiko cha fedha mdomoni, tukapata nafasi kwenye mazingira yaliyotufungulia milango ya mafanikio.
Wapo waliotoka kwenye
mazingira tofauti na wakaweza kufanya makubwa sana.
Amenifundisha kutokukata tamaa.
Nakumbuka mara ya kwanza alipofeli, kwa mara ya kwanza Frank alishtuka na kutambua kile nilichokuwa namwambia kila siku.
Akatambua kuwa makundi yanapita, baada ya shule kila mtu anashika njia yake
Aliporudia kwa mara ya kwanza, hakufaulu aliumia tena. Nikamsihi asiache, aendelee kukomaa hadi apate hicho cheti kitamsaidia huko mbele kielimu.
Hakuchoka kurudia hadi pale alipopata alichokuwa anakitafuta.
Wengi wetu, tunakata tamaa mapema.
Ila yeye, alijifunza kutokaan na
makosa ya mwanzo na kufanya vizuri zaidi.
Maisha ni safari.
Tupeane tumaini.
Wakati mwingine, inahitaji wewe kumuamini mtu na kumfahamisha unamuamini, kwa yeye kubadili maisha yake yeye mwenyewe.
Hakika, hujui nani atakuwa nani hapo baadae.
TUSHIKAMANE.
#DaktariMwandishi đź‘Ł
You can follow @Kudu_ze_Kudu.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.