Leo nimeikumbuka kesi iliyovuta watu wengi na ikapewa jina la KESI YA ZOMBE. Ilikuwa ni mwaka 2006 ambapo Dereva wa kampuni ya BIDCO alipiga simu polisi na kutoa taarifa kuwa amevamiwa na majambazi na kuibiwa pesa zote za mauzo.
Uzi
👇👇
Simu hiyo ilipokelewa CONTROL ROOM ya police na mpokeaji akasambaza taarifa kwa simu ya upepo juu ya tukio hilo. Taarifa hizo zikawafikia polisi waliokuwa sehemu tofauti. Tukio lilisemekana kutokea barabara ya SAM NUJOMA kituo cha KONOIKE
Polisi waliopokea taarifa hizo walikiwa sehemu tatu tofauti.
1. Polisi wa doria UDSM
2. Polisi kituo cha URAFIKI
3. Polisi wa OYSTERBAY na wote kwa nyakati tofauti wakaitikia kwenda kwenye tukio.
Walioanza kufika ni wa kituo cha URAFIKI ambapo walimkuta dereva wa gari inayosemekana kuvamiwa akiwa kapaki barabarani na akawaambia polisi kuwa waliomteka wamempora shilingi millioni tano,walitumia usafiri wa Toyota Mark II na wamepita njia ya SUPER STAR (Sinza)
Kumbukeni kesi hii inahusu mauaji ya watu wanne ambapo awali polisi walidai ni majambazi waliohusika na uporaji huo, Lakini wananchi walioiga kelele kuwa waliouwawa ni wafanyabiashara wa madini wa Mahenge. Kelele hizo zikamfanya rais mstaafu Kikwete aunde tume.
Kilichonivutia ni mmoja wa mashaidi wa upande wa mashtaka bwana SHABANI MANYANYA alipojitokeza mahakamani na kudai yeye ndie aliyepaswa kuuwawa na si marehemu kwani yeye ndiye aliyehusika na wizi wa BIDCO kwani dereva wa BIDCO ndiye aliwapa mchoro.
Dereva aliwaambia kuwa kila siku anakusanya mauzo na kuwa na pesa nyingi hivyo waunde tukio la uvamizi. Shaidi akadai kuwa yeye hafanyagi matukio ya siraha hivyo akawaleta vijana wawili na akaongezeka tingo wa gari ili kulinda maslahi ya dereva
Tukio likapigwa lakini walipata milioni 6 tu badala ya 36 walizotarajia hivyo shaidi aliambulia laki nne tu. Hata hivyo anasema baadae alifatwa na askari wa oysterbay na wakampukutisha laki tatu na nusu na akaambiwa akajifiche mpaka ishu ipoe
Alikuja kushangaa baadae anaona kwenye vyombo vya habari kuwa majambazi wa BIDCO wameuwawa wakati yeye muhusika na wenzake wanajua walishamaliza na polisi na wameshapukutishwa hizo pesa. Shaidi alidai ile huwa ni kawaida yao na akawataja waliompukutisha.
Aliuzwa swali na wakili wa utetezi kwa nini yupo uraiani na sio jela? Akajibu waulizwe polisi. Anasema aliamua kwenda kuhojiwa na tume ya Jaji Kipenka ili haki itendeke.
Kumbuka hawa wafanya biashara ya madini SABINUS CHIGUMBI aka JONGO na wenzake watatu walianzia safari yao mahenge kwenda Arusha kuwapeleka binti zake wawili shule,pia kuuza madini yanayokadiliwa kuwa na thamani ya milioni 200. Waliuza kiasi cha madini wakaja mpaka Dar
Walipofika dar walifikia BONDENI HOTEL. Ili kuweka sawa matukio mjue walikuwa na usafiri wao private na dereva wao(luteni mstaafu wa jeshi) alikuwa ni ndugu wa mmoja wa marehemu. Dereva huyu alikuja kuwa shaidi wa upande wa mashtaka baadae
Wakiwa dar waliuza tena kiasi cha madini na walikuwa wanatembea na fuko la hela. Walipeleka gari yao gereji na wakiwa huko mfanya biashara mwenzao akiwa mahenge aliwaomba waende sinza kwa mke wake wakampekee pesa kidogo za matumizi.
Kwa kuwa gari yao ilikuwa haijamaliziwa matengenezo(kupaka rangi) walikuwa wanatumia usafiri wa Tax aina ya Mark II ambapo dereva wake walikuwa wanafahamiana kwani walikuwa wanamkodi mara kwa mara.wakaenda sinza kupeleka pesa kwa shem wao

ITAENDELEA
Walipofika sinza walimkuta mke wa jamaa wao aliyekuwa akiitwa BENADETHA akaitwa chobingo na bwana SABINUS CHIGUMBI akampatia pesa shilingi elfu 30 ambazo aliagizwa na mmewe aliyeko Mahenge kuwa akampe mkewe na yeye atamrudishia wakirudi.
Wakati wanageuza gari kutoka mara wakavamiwa na polisi(wale wa UDSM) kwani gari yao ilifanana na ya tukio lililoriporiwa. Wakawatoa garini na walipowasachi bwana SABINUS CHIGUMBI akakutwa na bastora. Hapo polisi wakawaambia wananchi wasogee kwani wanakamata majambazi
Bwana SABINUS CHIGUMBI alijitetea kwamba ile ni siraha yake na anaililiki kihalali lakini hakusikilizwa. Wakapekua gari kwenye buti wakakuta briefcase walipoulizwa kuna nini wakajibiwa kuna pesa shilingi milioni tano. Hapo ikawa kimuhemuhe
Wakati haya yanatokea,BENADETA(aliyepelekewa pesa)aliyaona kupitia dirishani kwani bado walikuwa hajatoka kwake lakini aliogopa kutoka hata hivyo alimpigia simu mumewe aliyeko mahenge kumtaarifu kuwa rafiki zake wamekamatwa na polisi
Niweke wazi hawa jamaa wasingekuwa na viunganishi kafuatavyo lazima wote tungeamini ni majambazi
1. Benadetha
2. Dereva wao (luteni mstaafu)
3. Yule jamaa wa Mahenge
4. Muhudumu wa BONDENI HOTELI
5. Fundi garage
6. Ndugu wa dereva Tax
Wengine ni waliouziana nao madini Arusha na Dar kwani walitaja na pesa walizowalipa(zilikuwa nyingi) Pia polisi walijichanganya kwenye daftari la mtunza siraha. Walirudisha risasi kama zilivyo wakati walisema kulikuwa na majibizano ya risasi na majambazi.
Watunza siraha wa Oysterbay na chuo kikuu walikuwa mashaidi muhimu sana kwa upande wa mashtaka ambapo walidai walilazimishwa na mshtakiwa namba mbili(SP BAGENI) kubadirisha taarifa zai kwenye daftari. Pia walitoa risasi kadhaa zikalipuliwe ili kuweka mambo sawa
Kesi ilikuwa nzito na mashaidi walikuwa wengi lakini mmoja wa washtakiwa AFANDE LEMA akawaweka pabaya wenzake baada ya KUUNGAMA kwa mlinzi wa amani wa polisi akielezea ushiriki wake na jinsi ZOMBE livyotoa amri ya kuuwawa kwa wale wafanyabiashara.
Ungamo lake lilikuwa kwa njia ya maandishi na akaukana utetezi wake wote alioutoa awali. Ungamo hili likaletwa kama kielelezo na mshatikwa akawa ni shaidi wa upande wa mashtaka na akapangiwa siku ya kutoa ushaidi.
Hapa kina Zome na washtakiwa wengine walionekana kabisa nyuso zao zilisawajika kwani LEMA alikuwa anaenda kung'oa kiraka kwenye jeans ya bishoo, kwa msemo wa kileo alikuwa anaenda KUKANYAGA WAYA. hata wakili wao anaowatetea JEROME MSEMWA alishangazwa.
Bwana... Bwana... mnaosema hakuna uchawi,kwenye kesi hii ilionekana dhahiri uchawi upo. Bwana LEMA akaugua ugonjwa wa ajabu akaota mapele na akakata kauli. Alikuwa hawezi kuongea na alifia mahabusu akiwa hajawahi hata siku moja kutoa Ungamo lake mahakamani.
Hivyo hata maandishi yake yalitupiliwa mbali kama ushaidi kwani hakuwahi kufanyiwa CROSS EXAMINATION
Sasa nisiwachoshe mmoja wa mashaidi alikuwa ni Mkurugenzi wa mashtaka wa wakati huo ELIEZER FERESHI ambaye alikuwa ni katibu wa tume uliyoundwa na rais. Yeye alitilia mashaka kupigwa risasi watu wote za shingo wakati wanaruka ukuta wa posta kama ilivyodaiwa awali.
Alijiuliza ni vipi watu wanaoruka ukuta wote wapate majeraha sehemu moja? Pia hawakukuta hata damu eneo inayosemekana walikamatiwa. Pia hakuna hata jirani aliyesikia mlio wa risasi. Mashuuda walidai walikamatwa kwa amani na walifungwa pingu. Walikuwa bado hai sinza.
Hapa ikajengwa hoja kama waliweza hadi kufungwa pingu je kulikuwa na uhalali wa kutumia nguvu hadi matumizi ya silaha? Pia waliangalia umbali kati ya wapiga risasi na tundu lilikochimbwa ukutani wakabaini yalikuwa matundu ya bisibisi na sio risasi.
Zombe alileta kihoja kubishana na hoja hiyo(mkumbuke mahakama iliamia sinza kwenye ukuta wa posta) zombe akaomba aitwe askari wa doria wapige risasi waone tundu litakalotengenezwa. Pia mahakama ilienda Mabwepande walikouwawa wafanyabiashara.
Hatimaye siku ya hukumu ikawadia. Jaji Salum Masati akiwa mezani kwake aliasoma hukumu yenye kurasa 230. Alichambua vielelezo vilivyofikishwa,mashaidi na hoja za utetezi.
Kuna msemo wa kisheria unasema "THE COURT IS NOT YOUR MAMA" na hapa ulijidhihirisha. Yaani unapopeleka mashtaka mahakamani uwe umejipanga kuithibitishia mahakama pasipo kuacha mashaka yoyote juu ya tuhuma unazowasilisha(Beyond reasonable doubt)
Mahakama haiwezi hata mara moja kusaidia kutoa mashaka kwenye ushaidi wa mshitaki. Mahakama huwa inampa mshitakiwa BENEFIT OF DOUBT kuwa inawezekana hakutenda kosa(Presumption of innocence)
Kwa hiyo upande wa mashtaka huwa una kazi kubwa kuthibitisha mashtaka yake pasipo kuacha shaka yoyote(BURDEN OF PROOF). Mawakili wa utetezi huwa wana kazi ndogo tu ya kutia mashaka kwenye ushaidi unaoletwa dhidi washtakiwa
Hapa ndio utaona kesi ilianza na mashaidi mia lakini wanapanguliwa wanabaki kumi ambao ushaidi wao ni undisputed. Tukirudi kwenye kesi mshtakiwa namba moja alikuwa ZOMBE hapa ndipo upande wa mashtaka ulichemka.
Kulingana na uchambuzi wa JAJI MASATI mtuhumuwa namba moja ni aliyefyatua risasi na kusababisha vifo vya wafanyabiashara wale. Kulingana na ushaidi uliotolewa CPL SAAD ndiye aliyewapiga risasi watuhumiwa na mpaka siku ya hukumu hakuwahi kufikishwa mahakamani.
Pia Jaji aliona mgongano wa maelezo ya mashahidi juu ya mwenendo wa zombe siku ya tukio. Wengine walidai alikuwepo kituo cha Urafiki,Muhimbili mochwari,oysterbay na kwenye msafara wa rais katika muda mmoja.
Jaji alidai sio rahisi kwa mtu mmoja kutokea maeneo yote hayo katika muda mmoja. Lakini Jaji anasema Zombe ana ukweli wake anaoujua kichwani juu ya tukio hilo lakini kwa ushaidi ulifikishwa kwake unaacha mashaka mengi kumtua hatiani
Jaji alielezea labda upande wa mashtaka ungemshtaki zombe kwa kuwa alisaidia ama kwa cheo chake au amri zake kuuwawa kwa wafanyabiashara kesi ingemwelemea Zombe lakini kwa kumwita Mshitakiwa wa kwanza ndipo walipokosea
Hivyo Judge alimwachia Huru Zombe na wenzake na akaamuru atafutwe CPL ASAD afikishwe mahakamani. Upande wa mashtaka ulikata rufaa hata hivyo zombe alishinda rufaa zote mbili.
Wakati wa rufaa ni SP CHRISTOPHER BAGENI aliyekuwa OC CID wa oysterbay alikutwa na hatia akahukumiwa kunywongwa mpaka kufa.
Nilipata bahati ya kukutana na Zombe na kuongea naye mawili matatu nahisi mwaka baada ya kuachiliwa. Nilikutana naye bar moja inaitwa IMASCO karibu na uwanja wa taifa.
Jamaa anajiamini sana na anaonekana ni mtu wa mazoezi sana,kwani nilihisi mkono mkavu kweli kweli wakati tunasalimiana. Inaonekata akikukata kibao utakaa chini ujute.
Wakati wa kesi yake alikuwa hafichi sura yake kama watuhumiwa wenzake yeye alikuwa anaweka pozi mbele ya waandishi wa habari ili apigwe picha.
Pia alikuwa anahamasisha watu wajitokeze kwa wingi mahakamani akiwaambia waende wakajifunze sheria. Nahisi alijua tayari loophole itakayomtoa. Mwaka jana alichukua Form kugombea Ubunge wa Songea Mjini lakini alikatwa na Wajumbe.
You can follow @fbuyobe.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.