KUTOKA MAKTABA 📚

Pichani ni kitabu kinachojulikana kwa jina la "VOYNICH MANUSCRIPT" kitabu hiki kimegunduliwa mnamo mwaka 1912 huko kasikazini mwa Italia na wataalamu wa historia.

👉Wataalamu hao wanasema "Kinakadiriwa kitabu hiki kimeandikwa kwa miaka mingi sana 👇
Inasadikika kiliandikwa kwa miaka 500 iliyopita kwenye karne ya 15 lakini kwa miaka kilichoandikwa inasadikika kati ya miaka 1404 mpaka 1438"

👉Kitabu hiko kinatajwa kuwa kina kurasa 240 ila wana historia wanasema kitabu hiko hakijulikani lugha iliyoandikwa ila kuna baadhi ya 👇
Namba kwenye kitabu hiko zimeandikwa kwa lugha ya kilatini na mengine kwa kijerumani lakini ni (High German).

👉Inasadikika kitabu hiko kiliandikwa kwa mikono na tangu kipatikane mnamo mwaka 1912 kitabu hiko hakuna anayejua ni nani aliyekiandika kitabu hiko (Unknown) 👇
👉Lakini kwa mujibu wa maelezo ya tafiti za Nicolas Gibbs inaelezwa kuwa kitabu hiko kinaonekana moja kwa moja kimeandikwa na mwanamke. Kwa sababu picha nyingi zilizopo kwenye kitabu hiko ni za wanawake na picha hizo zinaonesha wanawake wakiwa wanaoga. Anaeleza kuwa 👇
"Watu wa zamani waliamini kuwa bafu/chooni ni tiba ya matatizo/magonjwa mengi"

👉Labda nikujuze tuu kwenye kitabu hiko picha nyingi zilizochorwa humo ni picha zile za wanawake baadhi ya picha zilizomo kwenye kitabu hiko ni picha za kibaiolojia na material ya karatasi za 👇
Zilizoandikwa humo ni karatasi aina ya "Vellum paper" ni zile karatasi ambazo zimetengenezwa na ngozi ya wanyama ni zile karatasi ambazo haziharibiki.

👉Na katika kitabu hiko kurasa zilizochorwa humo ni kurasa 20 tu kwenye kurasa 240.

👉Kupitia michoro iliyomo kwenye 👇
Kitabu hiko cha "Voynich manuscript" wanasayansi wamegundua baadhi ya mambo yaliyoandikwa kwenye kitabu hiko yanaelezwa yamekusudiwa baadhi ya haya yafuatayo ndani ya kitabu hiko zinazofika tano (5) tuzione hem apo chini 👇
1: The botanical devision (Michoro kuhusu mimea)

👉Inaelezwa kuwa katika kitabu hiko chenye kurasa 240 zina michoro ya mimea isiyojulikana, pamona na maandishi yenye lugha ambayo mpaka hivi haijatambulika ni lugha gani ambayo ilitumika kuandika katika kitabu hiko.
2: The astronomical division (Michoro kuhusu anga/nyota)

👉Pia ndani ya kitabu hiko kuna kunarasa nyengine zimechorwa michoro inayoonyesha mambo yasiyojulikana kuhusiana na masuala ya anga.

3: The biological devision (Michoro ya kibaiolojia)

👉Katika kitabu hiko kunaelezwa 👇
Kuna michoro zaidi ya 28 ambayo ipo ikiashiria michoro ya kibaiolojia hata hivyo michoro yake haijaeleweka inamaanisha nini kwani hata hivyo mpaka leo hakuna alieyeelewa tafsiri ya michoro hiyo hata lugha ya humo ndani ya kitabu.
4: The phermaceutical division (Michoro kuhusu madawa, kemikali na mambo ya kemia kwa ujumla)

👉Zipo pia baadhi ya kurasa ndani ya kitabu hiko ambapo kuna michoro ambayo inahusiana na masuala ya kikemia ambapo hakuna maandishi yoyote zaidi ya michoro hiyo.
5: The final division (Hitimisho ya kitabu hiko)

👉Huku kuna kurasa 24 za kitabu hiko, ila kurasa 23 ni kurasa ambazo zina maandishi pekee na kila aya ya kwanza ya kitabu hiko na inaanza na nyota (*) na kurasa ya mwisho kabisa ya 24 hakuna maandishi yoyote zaidi ya picha za 👇
Za funguo.

👉Labda nikujuze kitabu hiki kiligunduliwa na bwana "Wilfrid Voynich"(pichani) ambae jina lake kamili anaitwa "Wilfrid Michael Habdank-Wojnicz" jamaa alikuwa raia wa Polish na alizaliwa mnamo 12 Nov 1865 alikuja kukigundua kitabu hiko mwaka 1912 na alikuja kufa 👇
Mnamo 19 March 1930 nchini New York katika jiji la New York City.

MWISHO 🙏🙏

Please follow me @mkomonisti RT, comments kama umependekezwa nayo thread hii ✌

#MzeeWaVituAdimu

🚶🏼‍♂️🚶🏼‍♂️🚶🏼‍♂️
You can follow @mkomonisti.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.