TECHNOLOGY:
Bado naendelea kuona wanaoongeza ukubwa wa RAM kwenye simu hawako makini. Kwa mujibu wa althorithims zote za OS inatakiwa kuhakikisha walau CPU itumike kwa kiwango cha juu, kwe bize. Hivyo kuongeza ukubwa wa RAM naona ni kama mwisho wa kufikiri kwani sii kweli kuwa..
Tunahitaji RAM, mahitaji yake yalikuja tuu wakati tunatumia MAGNETIC DISK STORANGE mbazo speed ya kusoma na kuandika (R-W) ilikuwa ndogo sana. Ndipo wakafikiri wafanyeje ili walau CPU ipate kastorage ambapo katasaidia kuboost utendaji wa CPU. Lakini naona sasa baadhi ya makapuni
Hasa yale yale yaliyoamua kutumia android OS wanaona mpango mzima ni RAM. bila kijua kuwa kutumia RAM kubwa sii suluhisho la moja kwa moja, bali RAM bora yenye kuongeza uwezo wa R-W speed yaani kuanza kuunda kwa teknolojia kubwa zaidi kama ilivyo SSS (Solid State Storage).
UFAFANUZI WA CHANGAMOTO ZA RAM NA STORAGE
kumbuka CPU ndiyo ubongo wa kompyuta Tatizo kubwa ni kwamba Unapokuwa na CPU bora zaidi inakulazimisha walau uwe na RAM bora sana na ukiwa na RAM bora ni ili iweze na matakwa ya STORAGE yaani visiachane katika ubora na teknolojia
Kwa lugha nyingine CPU ikiwa bora sana ikapewa RAM nyenye uwezo mdogo ni kazi bure kwani CPU hulishwa na RAM hivyo itafanya yale RAM iliyoipta tuu. Sasa kila wakiwaza kuboresha RAM wanaaona RAM ikiwa best sana itashindwa kwendana na Storage System ambayo ni
NON-VOLATILE (Haifuti vitu chaji inapoisha)

Changamoto ya RAM, CPU NA STORAGE ilisababishwa na OS algorithms tuu ambazo kuna FIFO,LIFO, RR na zingine. Baada ya kuona RAM nayo bado haitatui swala la speed ndipo wakaanza na utaratibu wa kuwa na kitu kinaitwa CACHES...
CACHES ni file ndogo ndogo ambazo OS (Operating System) inazitumia mara kwa mara hivyo zinatunza mahali ili baadaye CPU isitumie muda murefu kwenye kwenye STORAGE kuzitafuta kumbuka haitumii muda mrefu sana kuseek lakini kumbukwa kwa komputer milliseconds 1 ni kubwa sana
ANDROID WANA TATIZO GANI

Android ambayo wengi wanaona ndiyo imewekwa kwenye simu nyingi wanazoziita za android kama vile Samsung, Motorolar, Xiomi, Oneplus na wengine kama kina TECNO. Hii android ilifanikiwa kwa asilimia kubwa sana kwa kiwa inatumia kenel ya Linux ambayo ni bora
Sana unazungumzia kenel bora ukilinganisha na ile ya Microsoft au ya Apple. Tatizo tuu android walikosea kwenye swala ya Synchronization ambapo ni namna gani kitu kimoja kitaweza kutumika na app zaidi ya moja bila kuathiri utendaji wa moja kwa moja. Hapa ndipo wao walifeli
Kwani inakuja kwenye app moja kutumia resources fulani kunakuwa na delay kubwa ambayo inayofanywa na PROCESS LOCKING kwani background apps zinakuwa nyingi kulitatua ndipo UKUBWA wa RAM unafanya kazi ili kuendelea kushikilia baadhi ya files zinazokuwa utilized at a time.
BACKGROUND PROCESSES
Hiki nako ndo kitu balaa sana unapozungumizia swala la RAM na CHAJI ya simu. Labda niguse kwa kifupi nini hasa maana ya background processes. Hizi ni app ambazo zinafanya kazi bila mtu kuwa anazitumia, zinakuwepo tuu ili kusikilizia baadhi ya vitendo.
Mwanzo kabisa Android ilikuwa inaruhusu background apps kama services tuu. Yaani vitu kama Notifications, Alarm, na OS yenyewe lakini baadaye wakaruhusu kila app iwe na background process ili iwe rahisi kuresume unapoibofya. Hapa nalinganisha na apple. Apple huwa hawana exit app
Hata kama wewe ni developer wa iOS hakuna sehemu apple inakuruhusu kuexit the app wanasema hiyo ni kazi ya OS. Endapo mtu atataka kuexit app kwenye apple mpaka atuhome home button kuclear app kitu ambao kina sababu yake ambayo ni kuhakikisha hakuna app itakayo ondoka bila OS kuwa
na taarifa na hiyo app imeondokaje. Sasa kwenye android OS wanaruhusu app karibu zote kuendelea kurun background hata kama mtu hatumii ili tuu imtahisishie mtumiaji kitu ambacho ni kizuri lakini kibaya. Kusubiri sekunde 1 au 2 app ifunguke ni bora zaidi kuliko kuiacha app hiyo..
iendelee kutumia CHAJI na RAM kwa saa 24. Ni heri kujipa muda wa kusubiri kuliko hiyo hasara ya RAM na CHAJI. Kitu ambacho Apple OS wao wameweza sana. Jiulize simu za apple zinaendelea kuwa na RAM za wastani tuu lakini bado utendaji wake unaendelea kuwa na ufanisi mkubwa sana
ukilinganisha na simu hizi zinazotimia Android. Bila kwenda mbali nitasema waundaji wa android na wale wanaotumia android kuunda simu zao kama vile Samsung na wengine wako kibiashara zaidi. Ndiyo maana hata camera zao sasa kama techno wana mpaka megapixels 64 wakati apple
Wana megapixels 12 tuu lakini borw zaidi ya hiyo 64. Wengi hapa wanatumia customers understanding kufanya biashara, wanaamini mteja akiona RAM ni 6GB basi atakimbilia kumbe hiyo RAM imejaa GARBAGES tuu na sii sifa.

IPHONE SII KWAMBA NI BORA ILA INABEBWA NA OS YAKE.
Napokea Mrekebisho na maongezo yenu
@TOTTechs , @JemsiMunisi , @AuxGrep , @AbilMdone , @chapo255
You can follow @asatayo.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.