1/25
◾️ " NDOTO ZA NYOKA AU MAJOKA NA MAANA ZAKE"◾️

👉 Uzi,
🔺Wengi tumewahi kupata ndoto ambazo moja ya wahusika wakuu ni nyoka, katika thread hii tutaangazia ndoto mbali mbali za aina hio na maana zake .
2/25
👉Kuota ndoto yenye nyoka, ni utabiri wa uovu katika aina na hatua zake tofauti tofauti.
👉Pia ni ishara ya kuzingirwa na maadui katika siku za usoni au matatizo.
3/25
🔺Ikiwa mwanamke ataota ndoto kwamba nyoka aliyekufa anamwuma hii inatabiri kwamba "atateswa na uovu wa rafiki anayejifanya kumpenda".
4/25
🔺Ukiota Nyoka wakigongana na kuanguka juu ya nyoka wengine, inatabiri kuwa kwenye maisha yako kutakua na mapambano, bahati na majuto.
5/25
🔺Ikiona umemwona nyoka ndotoni ukamwua kitendo hicho huonyesha kua utatumia kila fursa ili kuendeleza maslahi yako mwenyewe, au kuheshimu maslahi ya wengine na mwisho utafurahia ushindi dhidi ya maadui zako.
6/25
🔺Ikiwa utaota unatembea juu ya nyoka wengi , basi hii humaanisha utaishi kwa hofu na mara kwa mara utapatwa na Ugonjwa na watu pia watu watatafuta sana kuchukua nafasi yako katika moyo wa mwenza wako.
7/25
🔺Ikiwa umeota unatembea juu ya nyoka halafu wakakuuma hii inamaanisha utashindwa kuhimili ushawishi mbaya wa marafiki na maadui wataua biashara yako.
8/25
🔺Ikiwa umeota nyoka mwenye madoa ya kawaida anakukaribia kutoka kwenye mimea ya kijani kibichi, na unasogea pembeni haraka wakati anakukaribia, na baada ya kusahau tukio hilo unaona tena joka linakukaribia na kuongezeka ukubwa, mwishowe inachukua namna ya nyoka mkubwa,
9/25
na ikiwa baada ya juhudi nyingi , unafanikiwa kutoroka shambulio lake, na kuacha kuliona kabisa, inatabiri kwamba hivi karibuni utahisi kuwa umetengwa na kupuuzwa, na mambo yatazidi kuwa mabaya kwako na utakua mtu wa kunusurika ajali au kufilisika.
10/25
🔺Ikiwa utaona au kukanyaga nyoka wakati unapotembea au kuoga, inaashiria kwamba kutakuwa na shida mbele yako na pia unaweza kufukuzwa kazi .
🔺Ikiwa umeota nyoka akiuma watu wengine, hii inatabiri kuwa rafiki yako wa karibu ataumia na vitendo utakavyo mfanyia.
11/25
🔺Ikiwa katika ndoto umeona nyoka wadogo, inaashiria kuwa utawakaribisha watu katika maisha yako wenye ukarimu wa urafiki ambao watakuchafua kisiri siri na kufanya kazi kupindua matarajio yako yanayozidi kukua.
12/25
🔺Ikiwa umeota Nyoka akicheza na watoto, ni ishara kwamba haujajaliwa na Mwenyezi Mungu kutofautisha marafiki zako na maadui zako.
13/25
🔺Ikiwa mwanamke ameota kabeba mtoto mgongoni halafu anasikia saiti za nyoka "ssssss", inatabiri kwamba atashawishika kutoa idhini au ruhusa , tendo ambalo litaonekana kuwa ni zuri kwake, lakini atagundua baadae kuwa ameingiliwa na fitina ambayo maadui walimfanya aipende.
14/25
🔺Ikiwa umeota na kuona nyoka wakiinua vichwa vyao na kutokeza nyuma tu ya rafiki yako, inaashiria kwamba utagundua njama ambayo imeundwa kumdhuru rafiki yako na pia wewe mwenyewe.
15/25
🔺Ikiwa utafikiria kuwa rafiki yako yupo chini ya udhibiti wa nyoka hao, inaashiria kwamba mtu fulani mwenye nguvu ya kushawishi mambo maovu atatumwa kwa niaba yako (akitumia jina lako) ili kumshawishi rafiki yako.
16/25
🔺Ikiwa wewe ni mwanamke na unaogopa sana nyoka, hii inaashiria haki zako zitashambuliwa sana , lakini sheria pamoja na marafiki wenye ushawishi watakulinda!
17/25
🔺 Ikiwa utaota paka na nyoka wakicheza kama marafiki kunaashiria mwanzo wa mapambano makali katika maisha yako na inaashiria kuwa adui anajenga urafiki na wewe kwa lengo la kupata siri zako; pia ni ishara ya rafiki anaetaka kuhakikisha mambo aliyoambiwa kuhusu wewe,
18/25
Ikiwa utaona ishara hii kaa mbali na marafiki wanaojipendekeza kwako ili siri za maisha yako zibaki kua salama.
19/25
🔺 Kwa msichana mchanga kuota kuona nyoka ikitambaa na kupitia kwenye maua, inatabiri kuwa atasikitishwa mapema sana na mapenzi, na mazingira yake yatakuwa ya kusikitisha na ya kukatisha tamaa, ingawa kwa marafiki zake anaonekana kuwa na bahati kwake.
20/25
🔺 Ikiwa umeota mbwa akiua nyoka mbele ya macho yako hii inamaanisha kua unabahati ya kuwa na maisha mazuri maana maadui zako wanaangushwa mbele ya macho yako.
21/25
🔺 Ukiota Nyoka anaua Watoto wa mnyama yoyote yule hii humaanisha kua Adui yako ataumiza wengine wasiona hatia wakati akifanya juhudi za kukuangusha au kukuangamiza
22/25
🔺Ukiota nyoka anajikunja karibu na wewe na kukunyooshea ulimi, ni ishara kwamba utawekwa mahali ambapo hautakuwa na nguvu mikononi mwa maadui, na utashambuliwa na ugonjwa na matatizo mengine.
23/25
🔺Ikiwa utaamua kupambana na nyoka huyo basi hii inamaanisha kuwa utapanga mkakati ili kusaidia kupindua upinzani uliopo dhidi yako.
24/25
🔺 Ukiota nywele zikigeuka na kuwa nyoka, hii inatabiri kuwa matukio yanayoonekana kuwa ya maana kwako yatakufanya uwe na wasiwasi.
25/25
🔺 Ikiwa umeota nyoka anabadilika na kuwa maumbo yasiyo ya asili, utakuwa na magonjwa au shida ambazo zitaisha ikiwa zitatibiwa au kupatiwa ufumbuzi wa kawaida.

" Man cannot contradict the laws of Nature. But, are all the laws of Nature yet understood❓"
----End-----
You can follow @.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.