MPISHI ASIYETAJWA WA CHAKULA CHA MBINU ZA MOURINHO TOTTENHAM
UZI

Nilikuwa namfuatilia sana Mourinho katika interview zake kwenye analysis za mechi katika runinga ya Sky Sports baada ya kuchemka Man United, alikuwa ni mtu anayetaka sana kubadili aina yake ya ufundishaji...

Mara kadhaa nilimsikia akiwasifia waziwazi Jurgen Klopp na Pep Guardiola kwa aina yao ya soka, mwenyewe akiahidi kwamba atakaporejea watu wataona mabadiliko makubwa kwenye mpira wake, baada ya muda akapata kazi Tottenham.
Jambo la kwanza alijijua yeye mbinu zake hazipendwi kwenye soka la kisasa, alichokifanya katika msimu wa kwanza ni kuachana na Rui Faria aliyedumu naye miaka 17 na kuhakikisha anampata mkali wa kusoma mchezo na mkali wa mbinu, ndoano yake ikatua Lille ya Ufaransa ambako kulikuwa
na kichwa kimoja kinaitwa Joao Sacramento. Mreno huyu umri wake ni miaka 31 tu lakini kazi aliyofanya nyuma ya kapeti ni ya kutukuka sana, kila kazi unayoijua wewe ya kuifundi kwenye football huyu jamaa ameifanya, huyu jamaa ana Masters ya 'performance in coaching'
kwa Kiswahili sijui tunaitaje
ambayo aliipata Wales. Amekuwa Mkufunzi Mbobezi wa Udadisi na Mbinu wa timu ya Taifa ya Wales, amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Udadisi wa Mbinu wa Monaco kabla ya kuwa kocha msaidizi katika klabu ya Lille.

Sasa alipotua Tottenham, Joao Sacramento ndiye aliyempa mbinu mzee Mourinho za namna ya kuwachezesha Harry Kane na Son baada ya kuona mzee anawatumia vibaya. Harry Kane wa sasa anakuja deep sana, anacheza kumsaidia Son kufunga zaidi kutokana na kuwa sharp, ndiyo maana Kane...
amekuwa na assist nyingi msimu huu (11) kuliko msimu wowote na Son amekuwa mfungaji hodari, yaani wamebadilishana kazi.
Unaambiwa Sacramento ana ushawishi kwenye dressing room ya Tottenham kiasi kwamba masuala yote ya mbinu za kimchezo anaachiwa yeye amalizane na wachezaji, ...
Unaambiwa Sacramento ana ushawishi kwenye dressing room ya Tottenham kiasi kwamba masuala yote ya mbinu za kimchezo anaachiwa yeye amalizane na wachezaji, ...
kifupi Mourinho anapewa sana somo la soka la kisasa na bwana mdogo.
Chochote kinaweza kutokea kwa Tottenham msimu huu kwenye EPL, Europa League na makombe mengine lakini nyuma ya mafanikio atakayopata Mourinho Tottenham kutakuwepo na bwana mdogo anaitwa JOAO SACRAMENTO
END

*Correction* ...... Mourinho alikuwa anafanya analysis ya mechi na runinga ya beIN SPORTS