JE WAJUA 
JE USHAWAHI KUSIKIA STORI YA IGBO LANDING?
Kama unajua basi wengine hawajui basi wacha niwajuze twende sasa mtu wangu 
IGBO LANDING ni eneo lililopo huko GEORGIA nchini Marekani eneo lililobeba historia kubwa ya waafrika katika jitihada za kupinga utumwa

JE USHAWAHI KUSIKIA STORI YA IGBO LANDING?




Yaani hapa ndipo eneo ambapo watumwa waliotoka Afrika walijitoa muhanga kwa kujizamisha majini kama ishara ya kuupinga utumwa.
Mnamo mwaka 1803 boti iliyokuwa imebeba watumwa takribani watumwa 75 kutoka Afrika Magharibi hususani nchini Nigeria iliwasili katika pwani ya


ST. SIMONS huko GEORGIA MAREKANI watumwa ambao walikua wa kabila la IGBO baada ya kuwasili huko utumwani waliona bora kujiua kuliko kukubali na kuendelea kutumikishwa kama watumwa.
Baada ya kwisha kuwauwa wale manahodha wa kizungu na kuharibu ile boti waliyokuja nayo


Watumwa hao wapatao 75 na wao waliamua kujizamisha kwenye maji kwa lengo la kujiua.
Wakiongozwa na chifu wao huku wakiwa wamefungwa minyororo shingoni walijipanga msururu kuelekea ndani ya maji ya mto DUNBAR CREEK huku wakiimba nyimbo watu mbalimbali walijaribu kuenzi


Tukio hilo la IGBO LANDING ikiwa katika kukumbuka harakati zilizofanywa na waafrika katika kuupinga utumwa.
Mnamo mwaka 2002 wamarekani weusi waishio ST SIMONS waliandaa kumbukizi ya IGBO LANDING kwa kulitembelea ambako tukio lilifanyika.
Pia vilevile kuna wasanii



Ambao kupitia kazi zao walijaribu kulienzi tukio hilo mfano BEYONCE katika nyimbo ya "Love Drought" anaonekana akiongoza msururu wa watu kuelekea ndani ya maji hiyo imetafsiriwa kama kumbukizi ya tukio la "IGBO LANDING" video
Pia TONI MARRISON mwandishi ambaye nae aliwahi



kushindo tuzo ya Nobel katika fasihi naye ameelezea tukio hilo la "IGBO LANDING" kupitia riwaya yake ya "Song Of Solomon".
MWISHO by @mkomonisti
#MzeeWaVituAdimu


MWISHO by @mkomonisti
#MzeeWaVituAdimu


