LIFAHAMU DARAJA LA CHOLUTECA
"A BRIDGE TO NO WHERE" #UZI

Hii ni tafsiri isiyo rasmi ya sehemu ya makala iliyoandikwa na @prakashiyer katika gazeti la @bworldph
la tarehe 27April-10May 2020.
Sehemu nyingine ni muendelezo nilioufanya kutokana na mazingira yetu. Tiririka nao.
Je umewahi kulisikia daraja la mto choluteca?
Hata mimi sikuwahi kulisikia hadi linipopata habari zake hivi karibuni.
Hili ni daraja lenye urefu wa mita 484 kukatisha katika mto mkubwa wa choluteca uliopo katika nchi ya Honduras huko Amerika ya kati.
Eneo ambalo limekuwa likikumbwa na mvua kubwa, vimbunga na mafuriko ya ukubwa wa kila namna.
Kukabiliana na hali hiyo mwaka 1996 nchi hii waliamua kujenga daraja kubwa na imara katika mto huu ambalo litakuwa na uwezo wa kuhimili dhoruba za kila namna ambazi zimekuwa kikwazo hapo.
Kampuni maarufu na mashuhuri kwa ujenzi wa madaraja nchini japani ilipewa zabuni/ tenda ya kujenga daraja hili ambalo lilitarajiwa kuwa mhimili na tiba ya mafuriko na ukosefu wa miundombinu ya mawasiliano katika sehemu kubwa ya nchi ya Honduras.
Ilichukua takribani miaka miwili kukamilisha ujenzi huu wa kihistoria ambapo mnamo mwaka 1998 wananchi walianza kuruhusiwa kulitumia daraja hili ambalo kila aliyepita hakuweza kuificha furaha yake juu ya uzuri na uimara wa daraja hilo jipya ambalo lilikuwa kivutio kikubwa pale.
Lakini katika mwezi Oktoba wa mwaka huo huo 1998 mvua kubwa iliyoambatana na kimbunga kilichopewa jina la Hurricane Mitch viliipiga vibaya nchi hii.
Mvua kubwa ambayo ilinyesha kwa muda wa siku nne tu lakini ujazo wake ulikuwa ni sawa na kiwango cha mvua ya miezi sita nchi ile.
Mvua hii iliharibu kila kitu nchi ile, miundombinu, mazao, makazi huku ikikadiriwa kusababisha vifo vya takribani watu elfu saba (7000).
Madaraja yote yaliharibiwa vibaya sana nchi nzima isipokuwa daraja moja tu.
DARAJA LA MTO CHOLUTECA, hili halikuathiriwa kabisa na dhoruba ile.
Lakini kulikuwa na tatizo jingine, wakati daraja hili likiwa salama salmini, barabara zote zilizokuwa zinakwenda kuunganika na daraja lile zilisombwa na mafuriko bila hata kuacha alama kuwa kuliwahi kuwa na barabara zilizokuwa zinaunga kingo za daraja lile kuingia ama kutoka.
Lakini hili lilikuwa dogo, kubwa zaidi ni kwamba yale mafuriko yalikuwa yamebadilisha kabisa uelekeo wa mto choluteca na hivyo kupita pembeni kabisa ya lile daraja bila hata tone moja la maji kupita chini ya daraja.
Hivyo pamoja na daraja lile kuhimili dhoruba ya kimbunga kile...
na kuendelea kubaki imara baada ya pale lilibaki kuwa daraja "lisilopeleka popote"/ lisilo na uelekeo wala msaada wa kuvusha kwenda popote.
"A BRIDGE TO NO WHERE".

Hili ni tukio lililotokea takribani miaka 22 iliyopita lakini lina mengi ya kutufundisha miaka hii tunayoishi.
Dunia inabadilika kwa haraka na kasi ambayo hatuwezi kuidhania.

Mfano mzuri kabisa ni ugonjwa wa COVID 19 ambao kwa muda mfupi sana umebadili kila kitu na maisha yetu kwa ujumla, mabadiliko ambayo hakuna hata mmoja wetu ambaye angeweza kudhani kama yangetokea.
Mwaka jana muda kama huu hakuna aliyewahi kufikiri kama:
-Fainali za michezo mikubwa duniani kama EPL, La Liga, UEFA, Euro zingeweza kutochezwa kabisa ama nyingine kuchezwa bila mashabiki.
-Mashirika makubwa ya ndege na usafirishaji wa abiria yangepaki ndege zao bila kazi.
-Mahoteli makubwa, Vivutio vya watalii, maeneo mashuhuri kwa mikutano yasingekuwa na wateja na mikutano hiyo kufanyika kwa mitandao kila mtu akiwa kibandani kwake.
-Binadamu wangefikia sehemu ya kuogopana hata kupeana mikono na kusogeleana.
Kila kitu kilibadilika kwa muda mfupi.
Mabadiliko haya ndiyo yanaweza kutokea ghafla kwenye afya yako, kazi/ajira, familia yako, biashara n.k n.k.

Miaka 5 iliyopita usingeweza kuwaambia wahariri wa magazeti hapa nchini kuwa nakala za magazeti zitakuja kukosa soko hivyo waanze kujipanga maana habari zitakuwa mtandaoni
Kwa sehemu kubwa wengi wetu tumekuwa tukijipanga na kuweka nguvu kubwa ktk kutafuta ufumbuzi wa matatizo tuliyonayo lakini hatupotezi muda japo kuwaza kuwa matatixo yenyewe yanaweza kubadilika na ule utatuzi ambao tushayapatia usiwe na maana tena katika kutatua tatizo lile lile.
Sina uhakika kama viwanda vya barakoa na vitakasa mikono ambavyo sehemu kubwa ya soko la bidhaa zao ilikuwa hapa nchini vilijipanga kutafuta masoko nje ya mipaka ya nchi kwa kufikiri kuwa utatuzi wa tatizo la March/April unaweza kubadilika na soko la bidhaa hizi likashuka ghafla.
Kama hawakuwaza hivyo inawezekana wanaingia hasara kubwa sana kipindi hiki maana bidhaa haitoki sana.
Je tunajipa muda wa kuwaza kuwa mto unaweza kubadili uelekeo wake na daraja imara tulilojenga likawa halina maana tena ktk kutatua tatizo baada ya kutumia gharama kubwa?
Tukipata muda wa kuwaza hivyo kuna mahali tutajua tunapaswa kujenga kitu ambacho si imara tu, bali kinachoweza kwenda na upepo wa mabadiliko ya tatizo.
"Dont just think about building to last but also to adapt".
Kwa kufanya hivyo tutajikuta tumeua ndege wawili kwa jiwe moja.
Vinginevyo naweza kujikuta tumeachwa na daraja la Choluteca, daraja imara lakini lisilopitisha chochote wala kuvusha kwenda popote.
You can follow @ZakayoMmbaga.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.