HISTORIA YA RAIS BENJAMIN WILLIAM MKAPA, ZAO LA KWANZA LA UCHAGUZI WA MWAKA ‘95

Ukiachana na kwamba alikuwa Raisi wa Awamu ya 3, Pia kuna mengi usiyoyajua katika Maisha ya Mheshimiwa BENJAMIN W. MKAPA... Basi chukua muda wako Tuifahamu historia yake japo kwa ufupi...👇🍿THREAD
WILLIAM MKAPA alizaliwa 12 Novemba mwaka 1938 huko Ndanda(Masasi) mkoani Mtwara enzi hizo Tanzania ya leo inatambulika kama Tanganyika, Alipatia elimu yake ya Msingi kati ya mwaka 1945 hadi 1956 katika shule za Lupaso, Ndanda, Kigonsera na St. Francis Pugu College
Mwaka 1962 alihitimu Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda na SHAHADA YA KWANZA YA LUGHA YA KIINGEREZA,

Mkapa alitaka kujiunga na wizara ya mambo ya nje lakini kwa kuwa hakuwa na uzoefu ilibidi aingie kwanza Serikalini na alipelekwa kuwa District Officer Dodoma mwaka huo huo
Mwaka huo huo Aprili.....Agosti alikwenda Columbia University ili kusomea Foreign Relations course iliyompa kazi Wizara ya Mambo ya nje na Mwaka 1963 Alianza kazi wizara ya Mambo ya nje wakati ule wa enzi za Oscar Kambona
Binafsi siku ile nilipomaliza kusoma kitabu cha Marehemu Mzee Mkapa kitu cha kwanza kabisa kugundua ni kwamba Mkapa alitengenezwa na Mwalimu Nyerere, Kwani wakati ule Mwalimu yupo mwaka wa mwisho pale St. Francis Pugu College alimfundisha Benjamin katika somo la Kingereza
Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa Hotuba za watu maarufu au viongozi mashuhuri wa hapa nchini mwetu basi pasina na shaka ulishagundua utofauti uliopo kwenye Kingereza ya Mzee Mkapa na wengine, Turudi kwenye lengo....
Mzee BENJAMIN aliongoza awamu ya tatu kuanzia Mwezi Oktoba mwaka 1995 mpaka Novemba 2005, MKAPA ndiye rais wa kwanza kabisa kuchaguliwa chini ya Uchaguzi ulioshirikisha Vyama vingi vya siasa mara baada ya mfumo huo kurudishwa mnamo mwaka 1992
Wakati wa awamu ya Mkapa makamu wa rais alikuwa Ndugu Omari Ali Juma aliyeshirikiana nae mpaka 2001
kisha akapokelewa na Ali Mohammed Shein, Waziri mkuu wake akiwa ni Fredrick Sumaye...
MKAPA kabla ya kuwa Rais alishawahi kushikiria nyadhifa mbali mbali ikiwemo; Kuwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria mwaka 1976 kisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada mwaka 1982
MKAPA AMETUACHIA KIPI CHA KUMKUMBUKA NACHO?

1. MKAPA BRIDGE

Ukizungumzia madaraja marefu yaliyopo kusini na mashariki mwa Afrika basi ni lazima utalitaja daraja hili la Mkapa, linapatikana Ikwiriri, limekatisha mto Rufiji. Unaambiwa daraja hili lina urefu wa Mita 970
2. BENJAMIN MKAPA HOSPITAL

Hii hospitali inapatikana mkoani Dodoma, miongoni mwa hospital za kwanza kabisa kuwahi kuendesha upasuaji na upandikizaji wa figo, Mwaka 2015 hii ilishika rekodi ya kuwa hospitali ya pili Tanzania kufanya upandikizaji wa figo yani “Kidney transplant”
Katika Historia July 23, 2020 inajiandika kama siku ambayo Mheshimiwa Rais Benjamin Mkapa aliiaga dunia, Muheshimiwa Mkapa alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokua akifanyiwa matibabu.... (Taarifa zaidi zitakujia)
Tukisema tuorodheshe yote pengine hapata tosha hapa, Au hautatosha mida wako...Tuzidi kumuombea Shujaa huyu, Mtu makini sana Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi...Ameen
Ndugu zangu, Tangu hii ni Thread yangu ya kwanza kabisa kuandika mtumie japo dakika 2 kila mtu kutoa Mark juu ya Uandishi wangu

Hope wengi mmependa, Na kama umependa basi usisite kunipa Retweet kule juu kabisa ili iwafikie wengi. Kizuri kula na wenzako
You can follow @Festoleak.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.