Masaa machache yaliyopita China imetuma gari la kiroboti (Mars Rover) kuelekea ardhi nyekundu ya Mars. Gari hilo linaambatana na Lander pamoja na Orbiter (kwa pamoja kwenye picha yenye maandishi). Hii ikiwa ni safari ya kwanza ya Uchina kuelekea sayari nyekundu.
Kufikia anga la sayari hiyo, chombo hicho kitapunguza mwendo ili kuingia kwenye obiti na kisha kitagawanyika, Orbiter itabaki kwenye obiti, Lander itashuka ikiwa imebeba gari na kuifikisha ardhini. Kisha gari litateremka kuendelea na shughuli zake. EU walijaribu njia hii wakafeli
Itachukua takriban miezi saba kufika. Umoja wa nchi za kiarabu tayari wametuma chombo (Orbiter) kuelekea huko siku ya jumatatu na @NASA wapo tayari kutuma gari lao liitwalo Perseverance yaani “Ung’ang’anizi” wiki hii. Badala ya Lander, wamarekani hutumia Sky Crane kutua gari lao.
Dirisha la kusafiri kuelekea huko litafungwa mwezi huu. Dirisha lingine litakua mwezi wa kumi lakini tatizo ni kwamba wakati chombo kinafika, Dunia na Mars zitakua pande mbili tofauti za jua hivyo kusababisha ugumu wa mawasiliano kama nilivyoeleza katika #uzi uliopita.
You can follow @dr_dedreamer.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.