U.S SECRET SERVICE -
Huduma ya SIRI ya Marekani
.
Wamekuwa kwenye uso wa DUNIA kwa zaidi ya karne na nusu. WANAWAKE na WANAUME zaidi ya 7,000 wenye jukumu la kuwalinda viongozi wa kitaifa na familia zao. Wako tayari kupoteza UHAI kwaajili ya RAIS wa MAREKANI
.
thread - uzi
Huduma ya SIRI ya Marekani
.
Wamekuwa kwenye uso wa DUNIA kwa zaidi ya karne na nusu. WANAWAKE na WANAUME zaidi ya 7,000 wenye jukumu la kuwalinda viongozi wa kitaifa na familia zao. Wako tayari kupoteza UHAI kwaajili ya RAIS wa MAREKANI
.
thread - uzi

Ilianzishwa mwaka 1865 kama ofisi ndogo ndani ya Hazina na baadae mwaka 2003 ikaamishiwa kwenye kitengo kipya cha usalama wa ndani wa nchi. Wakati inaanzishwa takribani robo tatu ya fedha zote zilizokua kwenye mzunguko Marekani zilikua bandia hivyo walikuwa na jukumu moja...
...tu, kuhakikisha wanatokomeza fedha bandia. Miaka 2 baadae waliongezewa jukumu la kuwasaka na kuwagundua watu wanaofanya udanganyifu dhidi ya serikali; jukumu ambalo lilidhamiria kudhibiti wavunja sheria wote ikiwemo wanachama wa kikundi hatari cha kibaguzi - Ku Klux Klan...
...Jukumu la kulinda watu lilianza mwaka 1894 walipopata kandarasi ya muda kumlinda Rais Cleverland. Mwaka 1901 baada ya Rais McKinley kuuawa, Bunge liliamua Rasmi kuwapa "Secret Service" kazi ya kuwalinda Marais wa Marekani. Na mwaka uliofuata majukumu yote ya ulinzi wa Rais...
...yakawa chini yao. Mwaka 1908, Rais Roosevelt alipeleka maafisa nane wa "Secret Service" kwenda kufanya kazi kwenye idara ya sheria ya Marekani ambao baadae walikua na kutengeneza idara nyingine ya ujasusi maarufu kama FBI, baadhi ya majukumu ya Secret Service wakapewa FBI...
...na mwaka 1917, Secret Service wakabaki na jukumu la kudumu la kuwalinda Marais wa Marekani na familia zao. Mwaka 1950, baada ya jaribio la mauaji kwa Rais Truman, Bunge liliamua kutanua wigo wa kazi ya Secret Service na kuwapa jukumu la kuwalinda Marais wateule na familia...
..zao pamoja na Makamu wa Rais, Makamu wa Rais mteule na familia zao. Mwaka 1963, Baada ya Rais Kennedy kuuawa, ulinzi wa Marais uliimarika maradufu. Miaka 5 baadae Kaka wa Rais Kennedy aliuawa akiwa kwenye kampeni na kufanya Secret Service watanue tena wigo wa ulinzi na kuanza..
...kuwalinda wagombea Urais. Tangu kifo cha Rais Kennedy mpaka leo ni watu watatu tu chini ya ulinzi wa Secret Service waliowahi kufanyiwa jaribio la mauaji, kati yao ni Rais Ford na Rais Reagan. Mawakala wa Secret Service wamegawanyika kwenye makundi mawili; kundi la kwanza...
...ni maafisa wa kawaida wanaovaa sare na kundi la pili ni Mawakala Maalumu (Special Agents) wao hawavai sare. Ili kujiunga na huduma hii ni lazima uwe na shahada ya kwanza (Bachelor Degree) na unapitia kwenye mchujo mkali ambapo wanaangalia historia yako na watu wako wa karibu..
...wanaobahatika kupita kwenye mchujo huo wanaenda kwenye mafunzo ya wiki 9 kwenye kambi rasmi ya jeshi ya Glynco, Georgia. Maafisa wa sare shughuli yao inaishia hapo ila wale watakaochaguliwa kuwa mawakala maalumu huendelea na mafunzo mengine ya wiki 11 kwenye chuo maalumu...
...cha usalama huko Beltsville, Maryland. Maafisa wanaovaa sare wanapewa jukumu la kulinda ikulu pamoja na majengo muhimu ya serikali yaliyopo jijini Washington. Mawakala maalumu wao wanatumia miaka 8 ya mwanzo kuzunguka mitaani kukusanya taarifa ambazo pengine zinahatarisha...
...usalama wa Rais na Taifa kwa ujumla. Baada ya miaka 8, Mawakala maalumu wanapewa jukumu la kuwalinda watu mashuhuri ikiwemo Rais jukumu ambalo ni lazima wakala alifanye kwa miaka 3 - 5 baada ya hapo ataamua kama anataka kuendelea na ulinzi au arudi mtaani kukusanya taarifa...
...Ni AIBU KUBWA kwa Afisa wa Huduma ya siri kuwa HAI wakati anayemlinda kafa kwenye shambulio. Na ni HESHIMA kubwa kwa Afisa KUFA wakati wa shambulio ili kuokoa UHAI wa anayemlinda.
'MWISHO
'MWISHO