Thread : Full Muvie yenye KB 8
Electrical Engineer Jan Sloot (Dutch) alitengeneza system aliyoipa jina la Sloot Digital Coding. Mfumo huu ulimuwezesha kuhifadhi muvi kwa KB 8 tu, ambapo mfumo huo uliweza kuicompress muvi yenye ukubwa wa MB 500/1024MB mpaka KB 8. Endelea


Sloot, aliamua kupeleka project yake katika kampuni ya Philips 11 July 1999, lakini kwa bahati mbaya Sloot alikutwa amefariki pembezoni mwa bustani yake. Kifo chake kilisababishwa na Heart Attack siku chache kabla ya kufikia Muafaka na kampuni ya Philips ili kuuza System yake

Baada ya kifo chake, Source Codes za hiyo system zilikuwa zimefutwa na haikuwezekanika kuzirudisha mpaka leo. Floppy Disk nayo ilipotea katika mazingira ya utata na hawakuweza kuipata baada ya kuitafuta kwa muda mrefu.
Kama invention yake angefakinisha kuiuza, unadhani watu wangeweza kunua High storage devices ?