SAKATA LA MTEI
Edwin Mtei alikuwa gavana wa kwanza mtanzania wa BOT,akawa Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki na pia akawa waziri wa Fedha.1979 wakati wa changamoto ya uchumi,Mwalimu alifungua tena majadiliano na IMF akaomba paundi milioni 150,IMF Ikatoa masharti makali.
Edwin Mtei alikuwa gavana wa kwanza mtanzania wa BOT,akawa Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki na pia akawa waziri wa Fedha.1979 wakati wa changamoto ya uchumi,Mwalimu alifungua tena majadiliano na IMF akaomba paundi milioni 150,IMF Ikatoa masharti makali.
IMF iliiambia Tanzania kuwa inapaswa ishushe thamani ya Fedha yake,iruhusu ubinafsishaji wa mashirika ya Umma ili iweze kupewa paundi Millioni 150. Mwalimu alikataa masharti hayo japo Mtei alimshauri akubali.IMF ikatuma wawakilishi wake kuja kuzingumza na Mwalimu,Mtei akawapokea.
Mwalimu alikataa kukutana na wawakilishi wa IMF akasema yeye sio kivutio cha watalii.Baadaye Mtei akamuomba na akakubali kukutana nao Msasani.Kwenye kikao mwalimu akawaambia kuwa hayupo tayari kushusha thamani ya fedha ya Tanzania kisha kwa hasira akaondoka akawaacha peke yao.
Mtei anasema Mwalimu alimwambia kuwa hayupo tayari kuongoza nchi kwa kufuata maagizo toka Washington.Mmari aliyekuwa katibu wa Mwalimu anasema Mwalimu alimpigia simu Butiku akamwambia wageni hao wa IMF waondoke nchini siku hiyo hiyo.Mtei akawachukua wageni hao akaenda nao kwake.
Mtei akasema tukio hilo na mengine aliyowahi kutofautiana na Mwalimu yalimfanya aandike barua ya kujiuzulu,kabla hajaipeleka akapokea barua toka kwa Mwalimu akadai hakuifungua ila akaiwasilisha yake kwanza.Mwalimu akauliza kama ameisoma barua aliyompa,Mtei akajibu hajaisoma.
Mmari anasema Mtei alipokea barua ya Mwalimu ya utenguzi wake kisha akaenda kwa Mwalimu akiomba amruhusu aandike barua ya kujiuzulu ili isonekane kuwa ametengulia jambo litakalo chafua sifa yake.Mwalimu akakubali na Mtei akaandika barua.Baadaye Mtei alianzisha chama siasa CHADEMA