Leo niwaelekeze jambo flani ambalo wengi hawalifahamu

✴️Jinsi gani touch screen inafanya kazi

✴️Najua unatumia smartphone/tablet n.k lakini hujui touch screen ikoje na inafanyaje kazi na je kwa nini usitumie kitu chochote ku-touch kama plastic n.k

Fuatilia uzi taratibu
Jinsi gani touch screen inafanya kazi

Kwanza unatakiwa kuelewa kuwa touch screen ina sehemu kuu tatu (layers) ambazo hufanya kazi kwa pamoja na mfumo mzima wa simu

(a) toughened glass ( iliyopo huu)
(b) Capacitive Touch screen
(c) Display (OLED au LCD)
1 Tuanze na toughened glass

Hii inaitwa scratch resistant ipo kwa juu sehemu unapogusa na kidole chako kwenye simu, kuna kitu kigumu wengine huita kioo cha simu

Hiki kioo ni kigumu mara tano zaidi ya vioo vya kawaida hata simu ikidondoka still bado inaweza kufanya kazi vizuri
Ilihali kioo kimepasuka au kuwa na scratch

✴️Kwanini hiki kioo ni kigumu hivyo

Katika utengenezaji wa vioo vya simu wanatumia chemistry iko hivi

Wanachukua potassium nitrate wanachanganya na sodium katika temperature ya 400C kwa sababu potassium nitrates atom
ni kubwa kuliko za sodium basi zinachukua nafasi yake na sodium kupanda kwa juu (create layer) hivyo hutengeneza strong bond (uimara mkubwa) ndipo hutengenezwa kioo cha simu kwa ajili ya kulinda simu yako including touch screen and display pindi simu ikidondoka au mikwaruzo
2. Capacitive touch screen

Hii ndiyo inafanya kazi ya ku-sense na kujua kama touch imefanyika na imefanyika sehemu gani kwenye simu na kitu gani kionyeshwe (to be displayed)

Hii inajua kama kitu kilichogusa simu ni sahihi au siyo sahihi mfano umegusa simu kwa plastic
material basi haiwezi kudisplay chochote

Capacitive touch screen inafanyaje kazi

Tough screen ina vitu vitatu

(a) Top grid (juu)
(b) clear insulator (kati)
(c) Bottom grid (chini)

Top grid na bottom grid zinaunganishwa na Indium Tin Oxide (ITO)
Umeme unapita kwenye sehemu zote za simu katika mfumo wa electrons lakini hauwezi kufika kwenye Top grid sababu ya insulator katikati ( haipitishi umeme)

Badala yake zinatengenezwa Negative electric field (NEF) ambazo husababisha positive charges kuwepo kwa juu
Kwenye Top grid hivyo hutengeneza capacitors

Ukipeleka kidole chako kwenye kioo cha simu (screen) utagusa hizo capacitors, capacitors itasense kidole chako kwa maana kinapitisha umeme, capacitors itatengeneza fundo kwenye sehemu uliyogusa, hilo fundo linaitwa TOUCH
Touch zote zinakuwa identified na kuwa processed na processor ya simu kujua unatouch nini na nini kiwe displayed

Ndiyo maana simu inachemka unavyotumia sana kwa sababu ya reactions btn your fingers and phone capacitors

Kabla ya ku-display tuangalie phone display ikoje
3. Display

Hii ndiyo inaonyesha kila kitu kwenye screen yako na unaweza kuona maandishi, picha n.k kwa Rangi mbalimbali

Kuna Tekinolojia mbalimbali za display kama LCD na OLED

LCD ~ Liquid Crystal Display
OLED ~ Organic Light Emitting Diode

Tuangalie OLED
OLED ni Tekinolojia ya kisasa zaidi katika kuonyesha vitu kwenye Ubora mzuri ( quality display)

Najua mnapendea simu zioneshe vitu clear au picha za simu ziwe clear basi tumia simu zenye OLED display

OLED display ina takribani 3.3 million pixel grids
Ambayo hutengeneza 10 million microscopic light in term of RGB system ( uwezo wa kuzalisha rangi tofauti tofauti)

Primary colours ziko tatu tu
R - Red
G - Green
B - Blue

Rangi zingine zote huzaliwa kutoka hapo

Kila pixel huundwa kwa negative, emmisine na positive layers
layers ambazo hufanya kazi ya kuleta quality and clear colours

Naamini umeelewa 🙏🏼

Cc: @WizaraUUM @ict_commission @renatuswilliam1 @jaliluzaid @Mkuruzenzi @ITexpertTz @razaqdm01 @OlesakaJR @Niztz @njiwaflow @BanzaBiashara @EmanuelYohana
You can follow @TOTTechs.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.