Fahamu Kuhusu UTI: UTI ni kifupi cha urinary tract infection au kwa lugha rahisi maambukizi katika sehemu ya njia ya mkojo. Tatizo hili husababishwa na bakteria ambao huvamia njia ya mkojo na kuanza kuzaliana na hapo ndio malazi huanzia. #ElimikaWikiendi
Asilimia kubwa (80 - 85) ya UTI husababishwa na bakteria aina ya Escherichia coli (E.coli). Kufanya mapenzi kwa nguvu au na mwenza zaidi ya mmoja, Kutozingatia usafi (mwili + choo), kisukari na kuziba kwa njia ya mkojo zimeonekana kuwa sababu kuu za kuambukizwa UTI.
Bakteria anapoathiri sehemu ya juu ya njia ya mkojo ambayo ni figo kitaalamu huitwa pyelonephritis au kidney infection na anapoathiri sehemu ya chini ambayo ni kibofu huitwa cystitis au bladder infection.
Inaweza kuathiri sehemu ya uke au kwenye mrija wa mkojo (urethra).
Inaweza kuathiri sehemu ya uke au kwenye mrija wa mkojo (urethra).
UTI huwa na dalili kama maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, kusikia haja ya kukojoa lakini ukienda chooni mkojo hamna. Dalili za mabadiriko ya mwili ni kama vile joto au tumbo kuuma sehemu ya chini ya kitovu.
Wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kupata UTI kuliko wanaume na hii ni kutokana na maumbile yao ya sehemu ya siri, kwao inakua rahisi kwa bakteria kuingia kupitia njia ya mkojo. Lakini sasa tofauti na wanawake, Wanaume wanapopatwa na tatizo hili huwasumbua sana.
Kwa nini mama mjamzito anapimwa mkojo akienda clinic? Mtoto anapokua tumboni hukandamiza kibofu cha mama hivyo kupunguza nafasi ya kutunza mkojo kwa wingi ndio maana mama mjamzito anakojoa mara nyingi.
Kutokana na hali hii mkojo mwingi hubaki kwenye njia ya mkojo (urethra) hivyo ukikaa kwa muda huongeza uwezekano wa kupata UTI
Upimaji wa UTI kwa mama mjamzito ni jambo la kawaida kabisa (routine) katika kuhakikisha ana afya njema (afya yake na mtoto).
Upimaji wa UTI kwa mama mjamzito ni jambo la kawaida kabisa (routine) katika kuhakikisha ana afya njema (afya yake na mtoto).
Licha ya kupima UTI mkojo wake hupimwa pia protein, uwepo wa chembe za damu, sukari au kama una shida nyingine yoyote.
Sampuli inayotumika ni mkojo na Kuna vipimo vitatu, moja kwa kutumia hadubini (microscope) nadhani ulishawahi kuona daktari kaandika urine for sed, pili ni kwa kutumia kijiti maalumu (urinalysis) na mwisho kuotesha bakteria (bactetia culture) ambacho ndio bora
Unaweza kujikinga na UTI kwa kuboresha usafi wa mwili, kama una wasiwasi na mwenza wako nenda haja ndogo baada ya tendo, usivae nguo ya ndani kwa muda mrefu, kwa wanawake inabidi ufahamu namna ya kujisafisha baada ya kwenda maliwato.