Thread.
Jana Nilivyokuwa Safarini. Ndani ya Basi nikapata bahati ya kukaa siti moja na Mzee Mmoja Mfanyabiashara. Baada ya Utambulisho. Akaniambia "Nina Matatizo na Mke Wangu, Kuna Mambo Nahitaji Nikushauri Ili Usije Kupata Shida Baadae!
Jana Nilivyokuwa Safarini. Ndani ya Basi nikapata bahati ya kukaa siti moja na Mzee Mmoja Mfanyabiashara. Baada ya Utambulisho. Akaniambia "Nina Matatizo na Mke Wangu, Kuna Mambo Nahitaji Nikushauri Ili Usije Kupata Shida Baadae!

-Epuka Kuoa Mwanamke Aliye Zaa au Mwenye Mtoto, Kwasababu watoto au mtoto wake akikua kama si wako Mwanamke atahamishia upendo na kujiamini mno Kwa sababu ya Mwanae huyo. Hivyo basi atakuletea Dharau za Hapa na Pale angali akifahamu mtoto wake yupo na atamuangalia.
-Epuka Kuoa Mwanamke ambaye nyumbani kwao ni jirani na mnapoishi, Kwani hawa watu mkikorofishana kama kwao karibu atakwenda haraka iwezekanavyo. Hivyo kuoa mbali itambidi achekeche akili yake na ridhaa yako itakua muhimu sana akihitaji kuondoka.
-Kabla ya kuoa hakikisha umechunguza kwa makini Koo au familia anayotoka mwanamke wako, Koo nyingine zina visa mbalimbali vya kitamaduni ambazo kama hautokuwa makini mtaharibu uzao wenu au familia itapatwa na misukosuko.
-Hakikisha Mwanamke unayehitaji kumuoa hakupandi kichwani(Asiye na mdomo), yaani kila lenye uzuri yeye kwake baya. Ukimwambia hiki yeye atafanya cha kwake na kisha akikosea wala hasumbuki kukuomba ushauri anaendelea tu.
-Epuka kuoa mwanamke anayefata mawazo au ushauri wa watu wengine lakini wako anaudharau na kutoufanyia kazi kabisa. 'Hapa alinisisitizia sana mpaka nikaogopa' Aliniambia Duniani kuna hesabu mbili tu, Kujumlisha na kutoa hizo nyingine zote ni mbwembwe tu.
-Epuka kuoa mwanamke ambaye hamjui Mungu. Hapa aliniambia hatoongea sana, kwasababu Mungu ni kila kitu.
-Mwisho akanisisitizia epuka kujibizana na mkeo kama utajaliwa, Kama yeye atafanya hivyo wewe kuwa serious na mambo ya familia na hakikisha unahudumia familia inavyotakiwa
Haya yalikuwa maneno ninayoyakumbuka kutoka kwa mzee yule.
"AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO"
#Mhizika
Haya yalikuwa maneno ninayoyakumbuka kutoka kwa mzee yule.
"AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO"
#Mhizika